Add parallel Print Page Options

30 Hapo zamani watu hawakumwelewa Mungu, naye Mungu hakulijali hili. Lakini sasa anawaagiza wanadamu kila mahali kubadilika na kumgeukia Yeye. 31 Amekwisha chagua siku ambayo atawahukumu watu wote ulimwenguni katika namna isiyo na upendeleo. Atafanya hili kwa kumtumia mtu aliyemchagua zamani zilizopita. Na alithibitisha kwa kila mtu kwamba huyu ndiye mtu atakayefanya. Alilithibitisha kwa kumfufua kutoka kwa wafu!”

32 Watu waliposikia kuhusu mtu kufufuliwa kutoka kwa kifo, baadhi yao walicheka. Lakini wengine walisema, “Tutasikiliza mengi kuhusu hili kutoka kwako baadaye.”

Read full chapter